Mkurugenzi Mtendaji wa TALISDA Foundation, Dkt. Adolph Noya anawakumbusha wadau na marafiki wote ambao wangependa kushiriki katika maadhimisho ya siku ya JUMANNE YA KUTOA (GIVING TUESDAY) kwamba siku ya maadhimisho hayo inakaribia. Kwa hivyo watakaoshiriki wanakumbushwa kufanya malipo ya mchango wao wa kila mtu Tsh. 20,000/= mapema. Mchango huo ndiyo utakua ni kwa ajili ya kujisajili uweze kushiriki na kwamba huo pia ni mchango utakaotuwezesha kufanya maandalizi ya kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji wakiwemo Watoto walio katika Mazingira Hatarishi. Tafadhali tuma mchango wako kupitia Akaunti Namba 41502301106 Jina TALISDA Foundation, Bank NMB . Tunatanguliza shukrani kwa ushiriki wenu.